VYOMBO VYA HABARI;
Najua kutangaza habari ni taaluma yenu ila kuna wakati hamtendi haki kwani hamzingatii weredi kwani mnapenda kutangaza habari zao na kuzivalia njuga wakati hoja zetu wananchi mnazikwepa hoja za wananchi juu ya uwekezaji bandari.
Lakini hata msipozipa kipaumbele bado taarifa ya mtu kwa mtu na mitandao ya kijamii itafikisha hoja zetu na maamuzi ya walio wengi.

BUNGE/WABUNGE
Napata mashaka kuwa wengi wenu hamkupata ubunge kihalali je? Ninyi ni wenye akili sana (spika) kuwadhidi wengine kwani wanaohoji mitandaoni hawana haki ya kusikilizwa (sauti ya dharau nikasikia wakati wa kupitisha azimio la uwekezaji)
Kama mlipata ubunge kihalali mbona hamuwasikilizi wananchi,
Najifunza kitu kimoja kwa Magufuli kweli yeye alichauguliwa kihalali ndio maana alijali rasilimali za watanzania,

Mnapitisha azimio la makubaliano yasiyoonyesha ukomo wa mwekezaji halafu mwekezaji yeye amewawekea masharti yake ambayo mmejifanya hayaoni, mnadai yatarekebishwa wakati wa kuingia kwenye mkataba wa uwekezaji sasa mtarekebisha nini kama mmekubari kuwa kwa namna ye yote makubaliano hayata vunjika?
au mnazani mnakula na kipofu?
Tupo macho bora ufanyike uwekezaji kwenye bunge lakini sio bandari.

MSEMAJI WA SERIKALI
Kweli kazi yako ni kuisemea serikali hili natambua lakini hamjiulizi kwa nini wananchi walio wengi wameyakataa hayo makubaliano yenu na Dp world?
Unatuambia kuwa hayo ni makubaliano tu! kwani huoni kuna vipengele vyenye utata humo na mmevikubari?
Msizibe masikio na kuwapuuza wananchi (mbio za kilema hazitimui vumbi)
Binafsi naungana na wanaopinga uwekezaji kwenye bandari zetu vinginevyo makubaliano yatazamwe upya na sehemu zenye utata zibadilishwe.

WAZEE NA HEKIMA ZAO..! UMRI UMEENDA LAKINI ANA MANENO YA BUSARA